Sisi wanacheche tuna shauku kubwa ya kuchochea hisia za kipekee za watanzania kwa kuzalisha kripsi zenye ubora wa hali ya juu na bei nafuu nchini Tanzania
Dhamira yetu
Tumedhamiria kuwaletea nyakati za shangwe, furaha, sherehe, na burudani kwa pamoja - kupitia msisimko halisi utokanao na fleva za kipekee za kripsi za Chehe. Lengo letu ni kuchochea hisia na matamanio ya kuishi maisha kwa ukamilifu.
Je, upo tayari kujiunga na kusherekea kwa shangwe nasi ?
Hadithi ya Cheche
Viazi
​
Je, unajua kuwa asilimia 100 ya viazi vinavyotumika kutengeneza kripsi za Cheche vimelimwa kwenye udongo wenye rutuba wa Tanzania?
Tunashirikiana na wakulima wazawa kote nchini kupata viazi vilivyobora kwa ajili ya kutengeneza kripsi za Cheche.
Mara baada ya mavuno, tunachagua viazi vilivyo bora zaidi kwa ajili ya kusindikwa katika kiwanda chetu cha kisasa kabisa kilichopo Mapinga, Bagamoyo.
Kiwanda chetu cha kisasa kilichokidhi vigezo na viwango vya kimataifa huhakikisha kripsi za Cheche daima ni za kiwango cha juu, zilizo freshi na zilizojaa fleva!
Mchakato wa Uzalishaji
​
Viazi vifikapo kiwandani kwetu, wataalamu wetu hodari, hutumia uzoefu na ujuzi wao kuhakikisha viazi vinaandaliwa kwa umakini kwa ajili ya kutengenzea kripsi.
​
Kiwandani, viazi huchambuliwa, humenywa na hukatwakatwa kwa umakini ili kufikia unene unaofaa, ili kupata kripsi zenye kranchi ya kipekee ya Cheche kripsi.
​
Kisha, kripsi hukaangwa kwa umakini. Hatua hii inahakikisha kila kripsi inachukua kiwango sahihi cha mafuta, kufikia muundo wa dhahabu na kranchi inayotambulisha upekee wa kripsi za Cheche.
​
Baada ya kukaangwa, kripsi zilizoiva huchanganywa na viungo mbalimbali vya kipekee vinavyopatikana Tanzania kukamilisha mchakato ambao hufanya kripsi za Cheche kuwa za kipekee zenye kranchi bombastik Kwa umakini, uangalifu na ustadi mkubwa, kripsi hupakiwa kwenye vifungashio ili kudumisha ubora wake.
​
​
​